Kwa mujibu wa idara ya tarjama ya Shirika la Habari la Hawza, Hujjatul-Islam Sayyid Ahmad Iqbal Rizvi, Makamu wa Rais wa Baraza la umoja wa waislamu Pakistan, katika mkutano wa vyombo vya habari uliofanyika Islamabad, kwa kuashiria kuzingirwa miezi minane watu wa Parachinar, aliikosoa vikali serikali na taasisi husika kutokana na ukimya na kutochukua hatua, na akatoa wito wa kuchukuliwa hatua za haraka kwa ajili ya kuhakikisha usalama, kufunguliwa njia za mawasiliano, na kushughulikia migogoro ya kibinadamu katika eneo hilo.
Mwanachuoni huyu kutoka Pakistan, kwa kuashiria umuhimu wa kimkakati wa eneo hilo, alisema: “Parachinar ni moja ya maeneo muhimu zaidi ya nchi kwa upande wa kiusalama. Watu waaminifu, wenye ufahamu na waliostaarabika wanaishi katika eneo hili, ambao licha ya kunyimwa haki kwa miaka mingi, daima wamekuwa wakiiunga mkono serikali na hawajawahi kufanya hata tendo moja la kuvunja sheria.”
Akiwa na majonzi kuhusu kuendelea kwa kuzuiwa kwa njia za mawasiliano ya eneo hilo, aliongeza: “Sasa zaidi ya miezi minane imepita tangu watu wa Parachinar wazingirwe, lakini hakuna hatua yoyote madhubuti iliyochukuliwa na serikali ya shirikisho, serikali ya jimbo wala taasisi za usalama kwa ajili ya kufungua njia hizo. Hii ni katika hali ambayo katika maeneo mengine ya nchi, serikali hutoa mwitikio wa haraka hata mbele ya migogoro midogo kabisa.”
Maoni yako